25 Novemba 2024 - 14:38
Maha'tir Mohammad: Viongozi wa utawala wa Kizayuni wanastahili kunyongwa

Maha'tir Mohammad, Mwanasiasa mkongwe wa Malaysia, akijibu hukumu ya Mahakama ya "The Hague" dhidi ya viongozi wa utawala haram wa Kizayuni, alisema kuwa wanastahili wanyongwe.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bait (a.s), Maha'tir Mohammad, baada ya kutoa Hotuba yake kwenye Mkutano wa Kimataifa wa "Terengganu 2024" katika kuunga mkono uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kwa kutoa Hati ya kukamatwa kwa Netanyahu, Waziri Mkuu na Yoav Gallant, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa utawala haram wa Kizayuni wakiwa na anuani ya wahalifu wa kivita, alisema: "Wanastahili kunyongwa".

Aliutaja uamuzi huo wa Mahakama ya Kimataifa kuwa ni Uamuzi wa Haki, na akabainisha:

"Viongozi wa Israel ni wahalifu wa kivita kutokana na mauaji ya kimbari waliyoyafanya huko Palestina, na wanapaswa kuadhibiwa".

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Malaysia aliashiria kuwa: Kuua hata mtu mmoja ni jinai, na akaongeza kauli hii kwamba:

"Mauaji ya Waislamu elfu 44 Wanaume, Wanawake na Watoto ni jinai kubwa sana, na wawili hao (Netanyahu na Gallant) wanapaswa kuadhibiwa".